Wednesday, February 10, 2010

TAZARA UNDER INTESIVE CARE

“TAZARA UNDER INTENSIVE CARE”



Siku moja nilipokuwa nikifungua katika mtandao mmoja unaoitwa Wavuti na kukuta maada moja iliyokuwa ikielezea na kufananisha sisi watu wafrika hatujawahi kuvumbua (invention) ya kitu chochote, nilitafakari sana baada ya kupitia hoja za watu mbalimbali ambao pia walikubaliana nalo na kuongezea kuwa “sisi waafrika ni wazuri sana wa kuharibu vitu vilivyomalizwa tengenezwa” We are good at destroying rather than inventing and proper usage of what already made ..je ni kweli?
Ni wiki chache tu zimepita tuliposhuhudia viongozi wetu wa ngazi za juu kabisa mawaziri wa miundombinu,biashara na fedha wa Tanzania na Zambia kwa pamoja waliongozana kwenda Nchini China kuomba nchi hiyo iichukue (kushirikiana) na kuiongoza reli ya TAZARA baada ya kuwa juu ya mawe.
Inawezekana ukaona ni kitu cha kawaida tu, lakini kama ni mtu wa kufikiria zaidi kumbuka watu haohao wamewajengea reli tena ni kipindi China haijawa na nguvu kama ilivyo sasa ,bado baada ya miaka zaidi ya 40 ya Uhuru wana nchi yetu kweli tunaongozana kwenda kuomba “management” mmmmh hivi tatizo ni nini? Je ni kweli sisi ni waharibifu kama nilivyotangulia kusema? Nilitegemea baada ya kipindi hicho chote basi tungekuja na kujisifi kwamba tumefaidika vipi na TAZARA na mipango mizuri ya baadaye ,lakini cha kushangaza sasa Menejiment yote iko kwenye mawe ..mmh hii ni aibu kubwa ..mnakwenda kuomba msaada huku hata deni la zamani halijamaliza kulipwa , Hivi ninyi viongozi huwa hamuoni hata aibu mda mwingine ?? ? This is absolutely shameful to parade our weakness to the extent of calling in the Chinese to run Tazara. I cannot agree that out of nearly 70 million people in both Tanzania and Zambia there are no qualified professionals who can run Tazara professionally.

Ni bora viongozi wetu wakawa wazi zaidi kama kampuni halina tija wala faida kwa nchi je inahaja gani ya kuendelea kugharamia kitu kisichokuwa na faida?
Kuna maaeneo ya kuwekeza kwa wageni lakini sio mpaka hata maeneo nyeti ,bado hatujasahau kuwa tuna mgogoro na kampuni ya RITES kwa reli yetu ya Kati,Sioni umhimu wa wageni kuwekeza kwenye maeneo kama hayo.
Ni uchungu mkubwa sana na usioweza kuandikika hata kidogo ukifikiria mwongozo wanchi yetu kwani baada ya vitu kuendelea na kusitawi vitu vinachakaa na kukosa hadhi yeyote? Menejimenti nzima ya Tazara imejaa wizi mtupu kuanzia viongozi wake hadi hata askari polisi wanaosafirisha mizigo ndio wanaoshirikiana na wezi kupora mizigo na mafuta ya treni ,sasa nani atawalinda wezi? Inamaan sisi wenyewe kweli tumeshindwa kujiongoza wenyewe?? Tunataka mpaka Malaika wa Mbinguni washuke ili watuongoze? Basi tuombe ruhusu hata Raisi tuchague wa nje ya nchi ili atuongoze?? Kama wizi umejaa menejiment nzima je unategemea hata hao wachina watabadilisha nini??
Watanzania wenzangu ni wakati wa kubadilika kumbuka “nchi itajengwa na kusitawishwa na wazawa wenyewe” . Wawekezaji tunawahitaji sana lakini sio kwa kila kitu tutegemea wawekezaji…tutakuwa watumwa wa wawekezaji?
Kama ni pesa siwezi kulikubali hata kidogo ,kama Gavana anajenga nyumba ya 1.4bil gaharama ambayo ingetosha kujenga nyumba za kawaida zaidi ya 100 na wananchi wakaishi na kufaidi matunda ya nchi yao, leo pesa zote hizo zinafanyiwa anasa na mtu moja? Huu wote ni ulafi na ubinafsi mkubwa , ni wakati wa viongozi wa Kiatanzania kubadilika na kujali masilahi ya nchi zaidi ya wao wenyewe? Hata hao wachina mnaowakimbilia wamefikia hapo walipo ni kwa kujali masilahi ya nchi zaidi ndo maana sasa uchumi wao unaendelea kuneemeka tu hata katika kipindi hiki kigumu cha Mtikisiko wa Uchumu.
Ni huo huo ubinafsi wa viongozi wetu unaofanya kufanya mambo kisiasa zaidi katika kila kitu huku wakiona kanchi kanazidi kudidimia, msijidanganye kuangalia hivyo vikwangua jua dare s salaam basi mnasema Tanzania imeendelea ..tembea nje ya jiji na mikoani ndo utajua ni jinsi gani wananchi wanashida na wamejikatia tamaa na maisha ,kwani viongozi hawajui hayo???
Serikari kushindwa kuwatumia wasomi wananchi wake hilo ndo tatizo jingine kwani wanajali zaidi ulaji wao kuliko kujenga nchi , Hakika nchi haitaendela bila kuwa na mabadiliko ya kisayansi na utendaji maana mambo mengi yanafanywa kwa kufikirika zaidi ya vitendo. Wakati huo huo viongozi wako radhi kumpinga hata kumwangamiza yeyote msomi kama ataipinga serikari…..Ni wakati wa kuwatumia wasomi katika maamuzi yote…..Viongozi wetu wakumbuke siasa inanafasi yake na wanataaluma pia wananafasi yao, wala wasitegemee kuwa nchi itaendelea kama kila kitu kinafanywa kisiasa zaidi ya vitendo. Lazima ifikie kipindi serikari ijali na kuwatumia vizuri wasomi kwa ajiri ya maendeleo yetu ya leo na kesho.
Tupo nje na tunaona ni jinsi gani nchi za wenzetu zinavyotumia wasomi karibu kila kitu, na wasomi wanaheshiwa sana katika mawazo yao maana kila mara mwanasiasa hata kiongozi hata fanya kitu bila kupata au kuwasiliana na wasomi katika maeneo husika.
Tanzania inawezekana sana kuwa kama nchi za magharibi kwani kila kitu tunacho na uwezo upo kama tutafanya mambo kisayansi zaidi kuliko kisiasa zaidi.
Let us unite and build a livable place and better Tanzania.We learn from the past by looking forward for the future while living a charitable and caring for the present.


Mallaba Jr.
MBBS

No comments: