Sunday, February 28, 2010

Sakata la Viongozi wenye vyeti feki

Ni mtazamo wangu kama hawa mafisadi wa elimu kama wataachiwa nchi yetu haitafika popote zaidi ya kudidimia zaidi ya hata ilipo sasa.
Ndo maana tunaona mikataba mibovu karibu kila sekita kumbe mikataba mingine sio kosa lao bali ni ukosaji wa elimu husika katika kuongoza sekta hizo nyeti.
Nadhani wakati umefika kwa wizara husika kuchukua hatua kali na kufatilia hili suala ,mimi sitakaa kimya kamye mpaka tujue mwisho wake.
Wanatudanganya wamesoma, wanachukua rasilimali zetu zote na kujitajirisha bado tunaendelea kuwapa madaraka, jamani wataanzania tunamatatizo gani? Ama kweli sisi ni vichwa vya wenda wazimu.
Lazima ifikie kipindi tuseme basi sasa maana wanatunyonya kila kitu, tungefarijika sana kama wangekuwa wanajali hapa wananchi walio masikini lakini hakuna chochote.
Hili pia linanipa picha ya jinsi viongozi wengi wazee wamefanya kazi na Baba wa Taifa lakn hadi leo bado wanataka madaraka, kwa nini msituachie sisi vijana ? mnataka madaraka ya nini zaidi na umri wote huo ?au ni sababu mnajua leo vijana wengi wamekuwa na uelewa mkubwa na hawakubali kudanganywa tena?
Hata kama mtatukwepa kumbukeni kuwa Vijana wa kale sio kama wa zamani, na si mda mrefu tunakuja maana ninyi ni dhahiri kabisa umri unawakimbia kwa sasa.
And Jesus once said ”If the blind lead the blind, both shall fall in the ditch.”


Wahenga walisema elimu ni chanzo cha maarifa, on contrary to that also if the Education will be used inappropriately will be the source of disaster in particular society such as corruption, underdevelopment, lack of sustainability and better health services, decline in education system and an increase in the government dependence from donor contries e.t.c
Kama ni mwanasayansi utakumbuka some of the great scientist walipokuwa wanafanya utafiti wao na wanapokosa uhakika zaidi walikaa kimya kabisa mpaka wanapopata more convincing power ndo wanapublish ..mfano Charles Darwin on the EVOLUTION OF Man, na wengine hata waliuliwa kisa tu ni kukosa pointi za uhakika mfano mzuri ni a Galilei Galileo na Kikule aliyevumbua Benzene ....NOTHING COULD HAVE BEEN PASSED WITHOUT TOIL ...je hapa tunajifunza nini???
Inaonyesha wazi kama kila mtu angeachwa tu afanye anavyotaka leo tusingekuwa na mabadiliko makubwa ya kisayansi kama tulionayo kwa sababu hata theory za uongo zingepitishwa na sisi ndo tungekuwa waathirika wa kila kitu.
Kama kila kitu mfano ujenzi na electronics vinatumia theory ..je hivyo vitu tungekuwa navyo leo.Tatizo la sisi (samahani ila sio wote)watu weusi tunahali ya kutojali next generation,tunapenda ubinafsi ndo maana utaona Kiongozi mkubwa hajali kesho kutakuwa na nini bali yeye akishajaza tumbo lake leo yatosha.
For me I consider this to be the great disease and if Diagnosis will not be made early it will soon turns to Chronic and everything will be too late to amend.
Ni mimi mtanzania na mzalendo
Mallaba Jr.

No comments: