Friday, February 12, 2010

TUTATUMA WAGONJWA NJE YA NCHI HADI LINI

By Raphael Mallaba Jr

Ni miaka mingi sana wakati nikiwa kijana mdogo nilikuwa nikisikia tu kuwa wagonjwa Fulani wenye magonjwa mbalimbali wanapelekwa nje ya nchi kwa ajiri ya matibabu, aidha katika kipindi hicho katika mawazo yangu mafinyu nilijua kuwa Tanzania haina madaktari wakutibu magonjwa hayo au hakuna vipimo husika.
Kweli sana tuko karne ya 21 na taifa letu likiwa linasherehekea uhuru wake wa karibu miaka 50 lakini kila mwaka ninaendelea kusukia kuwa wagonjwa wanapelekwa nje ya nchi kutibiwa kama India na nchi zingine.Maswali yangu ni mengi sana ila siwezi kuyaandika yote katika hii makala moja ila yananipa wasiwasi sana wa hii nchi yangu Tanzania kwani ni aibu sana kwa taifa kutuma wagonjwa nje ya nchi kila mwaka utafikiri taifa halina madaktari .
Moja, je tatizo hakuna madaktari wa magonjwa hayo husika? Au je tatizo ni la hao madaktari kutojiamini na wanalofanya?Nasema hivyo nikimaanisha kuwa kama ni madaktari nauhakika kabisa wapo na wanaweza kabisa kutibu au kufanya upasuaji wa wagonjwa husika. Nakubaliana kipindi cha nyuma kulikuwa na upungufu sana wa madaktari wa upasuaji wa magonjwa ya moyo( cardio surgeon) lakini kuna madaktari zaidi ya 100 walimaliza masomo yao miaka miwili iliyopita nchini India na sasa wapo hapo hospitali ya Taifa ambao walikuwa wameandaliwa maalumu ili kuanzishwa kwa huduma za upasuaji wa moyo Muhimbiri.
Sasa bado kuna haja gani ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi?
Pili, Inawezekana wakasema tatizo ni vyombo vya huduma vya magonjwa husika labda havipo nchini mfano MRI,CT,Laparascopy,Endoscopy,and other Radiological Imaging.Kweli vyombo vingi vya kisasa ni gharama sana na hiyo ndo inayosababisha gaharama kubwa za matibu sababu kabla ya kupata diagnosis lazima kwanza upitie vipimo husika.Hivi vifaa nauhakika kabisa kwa mahospitali makubwa kama Mhimbili,Bugando, KCMC n.k vyote vipo labda kwa new generation vinaweza kukosa.
Hata kama havipo je serikari na wizara husika inamalengo gani? Je Tanzania itaendelea kuwa nchi ya kutuma wagonjwa kila mwaka nje ya nchi? Je mnatambua kuwa gharama za mamilioni manazotumia kila mwaka kutuma wagonjwa nje ya nchi si zaidi ya miaka miwili vifaa vyote mhimu vingeweza kununuliwa?na watu hao kuendelea kutibiwa nyumbani kwa gharama nafuu kabisa?
Tatu, Kwa nini tuwe wategemezi kila siku au ni kutojiamini kwetu ndo kunakosababisha haya yote ?
Kama hakuna mda maalum wa kusitishwa kutuma wagonjwa nje,basi hili litakuwa ni dili la watu wakubwa maana kila wanapotuma wagonjwa kunakuwa na percentage yao wanayopata kwa hiyo kazi hii itakuwa ni ya kudumu,hata kama kuna madaktari na vifaa vya kutosha bado wagonjwa watapelekwa nje ya nchi.
Hii ni aibu sana kwa nchi na madaktari nchini kwani inaonyesha kuwa tatifa zima halina madaktari bingwa wakuweza kutibu wagonjwa wao.
Inanikumbusha siku moja rafiki yangu alikuwa akipata matibabu nchini China na madaktari wakamuuliza je nchini kwenu hakuna madaktari wa kumfanyia hii operation au hamna vifaa? Lilikuwa ni swali gumu sana kwangu ukizingatia gharama nchini China ni ghari sana ukilinganisha na nyumbani.
Naomba waziri wa afya na wizara husika ilifikirie kwa undani hili swala, kwani nilazima ifikie mahali mabo ya kuzoeleka tuyaache kabisa na tufanye vitu vyenye tija kwa taifa letu. Au mnataka hili nalo mpaka aje mwekezaji kutoka nje awaambie ndo mkumbuke kuwa uwezo mnao??

God bless Tanzania

Raphael Mallaba Jr.
drmallaba@yahoo.com
P.R.CHINA.

1 comment:

Anonymous said...

Ndugu mallaba Hongera kwa makala yako,ila bado kazi ipo kwa serikari yetu maana viongozi hawana uchungu na nchi yetu kabisa